Thursday, January 10, 2013

AUCHEBLOGSPOT:Mapenzi ni asali, ni shubiri, vaa moyo imara


Mapenzi ni asali, ni shubiri, vaa moyo imara Kwa nini mapenzi ni tata? Unaweza kujiuliza swali hilo. Ni kwa faida ya kila mmoja kwa sababu yanamhusu kila mmoja wetu. Ni matamu lakini ndani yake hutokea kuwa na ukakasi kama siyo maumivu. Jiulize tena, kwa nini mapenzi yanasumbua? Mapenzi ni maumivu ya kichwa na moyo. Watu wengi waliomo ndani yake wanaweza kukupa ushuhuda wa mateso wanayoyapata kwenye uhusiano wao. Je, baada ya kuteseka huwa wanajiapiza kutorudi tena? La hasha! Wanajaribu mara nyingi, hawakomi. Unaweza kujiuliza ni kwa nini lakini ukweli ni kwamba pamoja na maumivu ambayo mtu anaweza kuyapata kwenye mapenzi, bado yanabeba hisia kubwa kabisa katika maisha ya kila binadamu. Maisha bila mapenzi hayajakamilika. Kutokana na hilo, uwanja upo wazi kwako kujiuliza ni kwa nini kitu kitamu namna hiyo kikafanywa kuwa tata, jumlisha na maumivu ya hapa na pale. Uvumilivu ukizingatiwa, huyeyusha utata unaojitokeza hapa na pale. Muhimu zaidi ni kwamba mapenzi hayatoshelezi kwa uwajibikaji wa nusu nusu. Yanahitaji nidhamu na utekelezaji wa moja kwa moja kutoka moyoni. Yanayomhusu mwenzi wako ni vema uyabebe kama yako, hivyo ndivyo uhusiano unavyotaka. Mapenzi yanahitaji akili, utashi na fikra zako bila kusahau nguvu zote katika kuzalisha matunda ya kila siku kwenye uhusiano ulionao. Utata unaoonekana ni ule unaotokana na wenzi kutotimiza matarajio ya kila mmoja. Imetokea kuamini kuwa maneno ni mhimili wa kudumu kwa uhusiano na ngono husuluhisha migogoro ya muda mfupi. Wapenzi wanaponuniana, endapo watakutana faragha, hasira zote huspotea. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, ni zaidi ya kutosheka kimwili na utamu wa maneno mazuri. Kwa mfano, ndoa nyingi zinakumbwa na matatizo ya watu kushindwa kuwa wakweli. Mwanaume au mwanamke anaweza kusema ni kiasi gani mwenzi wake anamuumiza. Lakini mwisho wa mazungumzo hawezi kukiri kasoro zake ambazo pengine ndiyo chanzo cha kila kitu. Utata zaidi katika mapenzi ni kuwa inapotokea watu wanajuana kwa undani mno, hasa baada ya kuishi muda mrefu, ni hapo ndipo maneno hayawezi kufaa kitu, wala mchezo wa faragha hautaleta maelewano kwa maana hakuna kitu kigeni. Lingine la utata katika mapenzi ni kwamba huwezi kuficha tabia yako muda wote. Ukishazoeana na mwenzi wako hasa baada ya kuwa pamoja muda mrefu, utaanza kujiachia. Ni kipindi ambacho mmoja anaweza kuhisi amesalitiwa kwa sababu mwanzoni hakuona hivyo ‘vitabia vya kuudhiâ €™, alifichwa.

Monday, January 7, 2013



"Kwa Mara ya Kwanza Nchini Tanzania .... Jifunze Sound na Swaga za Kijanja za Kula Mzigo Fasta,


Kutongoza ni sanaa ya ushawishi, ambayo lengo lake ni kula mzigo. Kuna sanaa zingine za ushawishi kama vile ushawishi wa kibiashara ambapo lengo ni kuuza bidhaa. Na kuna ushawishi wa kisiasa ambapo lengo ni kupata kura. Wakati sanaa karibia zingine zote za ushawishi ni rahisi kujifunza, sanaa ya kutongoza watu wengi wanasema eti haifundishwi ... eti kila mwanaume anajua kutongoza. Sio Kweli !!! Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza, kwa sababu kuna mwanaume anaweza akongea na demu mpya leo na akala mzigo leo leo, au akichelewa sana basi ndani ya wiki moja; wakati huo huo kuna wanaume wengine wanahangaika miezi au hata miaka kula mzigo. Au wengine wanatoboka sana mifukoni .... unakuta mtu anampangishia demu nyumba, au anamlipia ada ndio ale mzigo. Wakati huo huo kuna wengine wanakula hapo hapo bure, tena bila kunawa! Wanawake ni watu wa vikwazo. Wenyewe wanasema wanaweka vikwazo ili kukupima kama una "mapenzi ya kweli". Unachotaka wewe ni kimoja. Kula mzigo. Maana inabidi ule mzigo kwanza, ndo ujue kama uendeleze mapenzi yawe ya kweli ... au upotezee. Au sio mzee? Ila yeye atakuwekea vikwazo kibao kama vifuatavyo: Niko kwenye period Nina boyfriend / mume / mchumba Ninaumwa (malaria/tumbo/ kichwa/n.k.) Mama yangu mgonjwa Niko bize na kazi Nimeokoka nampenda Yesu! Mwanaume wangu ni Yesu tu! Wiki hii nina test (kwa wanavyuo) Mi sitaki mambo hayo, mpaka nimalize masomo nipate na kazi Mi bado mdogo Sitaki!! Nyumbani kwetu geti kali siwezi kutoka Wewe sio mwanaume wa type yangu (mfupi sana/ mweusi sana/mweupe sana/ huna hela/n.k.) Mi sitoki/siongei na watu nisiowajua (strangers) Sijisikii kuwa na wewe / sikupendi! na kadhalika Je ni mara ngapi umekwamishwa na mojawapo ya vikwazo kama hivyo hapo juu? Utajisikiaje nikikwambia kuwa vikwazo vya dizaini hiyo vingi ni geresha tu ... sio vikwazo kwa maana ya vikwazo bali ni fursa nzuri kwako kupata unachotaka? Na bomba zaidi je unajua mbinu za kutumia ili kumfanya mwanamke asikupe kabisa vikwazo kama hivyo? Ukimtongoza mwanamke vibaya atakuwekea vikwazo vingi na hata kama utampata atakuwa ashakuzungusha sana na kukupotezea muda na pesa. Ukiwa na mbinu za kuzuia vikwazo maisha yako yatakuwa rahisi zaidi.